DStv Inogilee!

Kifaa kipya cha Simba kutua leo kuziba pengo la Shomari Kapombe

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC hii leo wanatarajia kumpokea beki wao mpya kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Zana Coulibaly atakayeziba pengo la Shomari Kapombe.

Kupitia mtandao wao wa kijamii wa Instagram, Simba imethibitisha juu ya ujio wa beki huyo wa kulia raia wa Ivory Coast.

Tunapenda kuwatangazia kwamba beki Zana Coulibaly kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast leo atawasili nchini kwa ajili kukamilisha taratibu za mwisho kujiunga na timu yetu ili kuziba pengo la beki Shomari Kapombe ambaye siku za karibuni alipata majeraha.

Mbali na ujio wa nyota huyo miamba hiyo ya soka ya Tanzania hii leo itakuwa na kibarua kizito pale uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo itamenyana na Mbabane Swallows katika kutupa karata yao ya kwanza kwenye michuano ya hii klabu bingwa barani Afrika.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW