Michezo

Kifaa kipya Yanga hiki hapa, ni hatari tupu, aitumikia klabu yake msimu mmoja tu na kuwa kinara wa mabao, kutua nchini mwezi ujao

Kwa mujibu wa mtandao wa michezo wa ‘Kawowo Sports’ kutoka nchini Uganda umeripoti kuwa mshambauliaji wa zamani wa klabu ya Onduparaka FC, Agau Rashid ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Maroons FC anatarajiwa kuwasili Tanzania mwezi Juni kwa ajili ya majaribio katika miamba ya soka ya ligi kuu Young Africans SC.

Rashid ni mzuri wa kumiliki mipira na mfumaniaji mzuri wa mabao 

Kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo, amesema kuwa Agau amepata mualiko kwaajili ya kwenda kufanya majaribio kufuatia kufanya vizuri zaidi msimu huu.

Nyota huyo wazamani wa Onduparaka, amejiunga na Maroons msimu wa mwaka 2018/19 akiwa kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka mitatu hata hivyo kama atajiunga na Yanga atakuwa amewatumikia waajiri wake hao mwaka mmoja pekee.

Ndani ya msimu huu mmoja, Agau Rashid amefanikiwa kufunga jumla ya mabao saba na kuwaacha mbali baadhi ya wachezaji wenzake kama Pius Obuya na Seif Batte wenye mabao manne kila mmoja ikiwa pamoja na Isaac Otto, Bronson Nsubuga waliyosajiliwa msimu huu mwezi Januari wakiwa na mabao matatu.

Klabu ya Maroons imetoa baraka zote kwa, Agau endapo atafanikiwa kufuzu majaribio yake ndani ya Yanga, hata hivyo kama atafanikuwa atajiunga na baadhi ya Waganda wenzake kama Emmanuel Arnold Okwi na Murushid Jjuuko wanaotumikia klabu ya Simba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents