Michezo

Kifo cha mchezaji, Cheick Tiote kinaniumiza – McClaren

Aliyekuwa meneja wa zamani wa klabu ya Newcastle, Steve McClaren amesema anamkumbuka sana mchezaji Cheick Tiote kwa tabasamu lake katika mchezo wa mpira wa miguu,
Meneja huyo ameyasema hayo mara baada ya hapo jana mchezaji Cheick Tiote kufariki dunia wakati wa mazoezi nchini China, alipokuwa akichezea soka lake la kulipwa akitokea katika klabu ya Newcastle mwezi wa Februari.

Aliekuwa mchezaji wa klabu ya Newcastle, Cheick Tiote enzi za uhai wake

McClaren, “Tiote ni mchezaji imara na mwenye tabasamu zuri ndani ya mchezo wa mpira.
“Ndani ya klabu ya Newcastle nikiona tabasamu la wachezaji, Papiss Cisse pamoja na Cheick natambua hapo dunia ipo salama,” McClaren aliiambia BBC 5 .

“Yeye ni aina ya mchezaji ambae kila mtu anatamani kuwa naye katika timu.”
McClaren, ambaye alikuwa meneja katika kikosi cha vijana na wakubwa ndani ya klabu ya Newcastle, aliongeza kuwa “Nilianza kumfahamu kwa mara ya kwanza katika kikosi cha vijana ni mchezaji imara ambaye sijapatakuona”

Aliekuwa meneja wa  klabu ya Newcastle, Steve McClaren

“Ndani ya mchezo na katika mazoezi huonyesha juhudi, alikuwa anahitaji kushinda kila mchezo.
“Zilikuwa ni ndoto zake kucheza nchini China na nilifurahi baada ya kuona amefanikisha hilo, alikuwa akikusanya fedha kwaajili ya kuisaidia familia yake.

“Alikuwa akicheza ili kuweza kupata fedha za kuisaidia familia yake, wajomba zake, shangazi zake, babu zake na wale wote waliokuwa wanamtegemea.

Aliekuwa mchezaji wa klabu ya Newcastle, Cheick Tiote enzi za uhai wake

Anakumbukwa sana ile siku ambayo timu yetu ya Newcastle ilipotoka nyuma ya magoli 4 kwa 0 katika mchezo wetu dhidi ya Arsenal mpaka tuka suluhu kupitia goli lake hodari.

“Nilimpenda sana. Yeye ni kilakitu ambacho ungekihitaji kama mchezaji ndani ya klabu ya Newcastle.
“Wakati mwingine maisha hayatendi haki kabisa na nitamkumbuka Cheick Tiote kama kiungo niliyewahi kumpenda.
Pumzika kwa burihani rafiki yangu.” Alisema McClaren

Tiote alizaliwa Ivory Coast na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents