Burudani

Kifo cha Oliver Mtukudzi chakatisha ndoto za Linex ‘naongea na watoto wake, aliniahidi kuja Bongo turekodi’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Linex amefunguka kuwa alikuwa na mpango wa kufanya kolabo na marehemu Oliver Mtukudzi kutoka Zimbabwe.

Linex kulia akiwa na Mzee Mtukudzi kati kati.

Linex akihojiwa kwenye kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushhwa na kituo cha Radio cha E-FM, amesema kuwa Mzee Mtukudzi alikuwa ni mtu wa karibu sana na yeye kwani licha ya kusubiri kolabo hiyo, lakini pia alikuwa na mawasiliano ya karibu na familia ya Mtukudzi.

Akiongelea kuhusu kolabo, Linex amesema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili walikuwa wameshapanga ila ni nafasi tu ndio ilikuwa haipatikani kwa upande wa Mtukudzi.

Linex amedai kuwa mwaka jana kuna kipindi, alimuomba japo aingize sauti akiwa Zimbabwe halafu amtumie, lakini marehemu Mtukudzi alimwambia asipate tabu kwani atakuja mwenyewe hapa Tanzania kurekodi naye.

Siku aliyofariki Oliver Mtukudzi Januari 23, 2019, kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika “Rest a peace papa ya Muziki Umeondoka kabla sijakamilisha ndoto ya kurecord na wewe 😭 japo tayari Ulikua umeshakua rafiki Yangu unanitania na kutania Mungu akulaze kwa Amani pole Sana @jackiengarandeofficial na Familia kwa Ujumla Bwana aliekutoa hatimae amekutwaa Jina lake Lihimidiwe 🙏 Papa You gonna lieve inside me Forever”.

Linex mwaka huu, ameufungua vizuri kwa kuachia wimbo wake wa Too Late ambao amemshirikisha Lady Jaydee, usikilize hapa chini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents