Habari

Kifo cha Profesa Maji Marefu chamuibua Dkt. Mwigulu Nchemba

Kufuatia kifo cha Mbunge wa Korogwe vijijini (CCM), Stephen Ngonyani almaarufu kama Profesa Maji Marefu kilichotokea usiku wa jana, kimemuibua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Image result for Mwigulu nche,mba na MAJIMAREFU
Dkt. Mwigulu Nchemba

Mwigulu ambaye amevuliwa uwaziri na Rais Magufuli wikiendi iliyopita amesema kuwa CCM imepata pigo kwa kumpoteza kada na kiongozi wa kweli.

Maandiko matakatifu yanasema, Mwanadamu aliyezaliwa na Mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, Tumempoteza kaka,ndugu na rafiki Comrade Stephen Hilary Ngonyani (Prof.MajiMarefu), tumempoteza Kiongozi na kada kweli kweli wa Chama Cha Mapinduzi.“ameandika Mwigulu Nchemba kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Profesa Maji Marefu ameaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Soma zaidi taarifa ya kifo chake HAPA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents