Shinda na SIM Account

Kifo cha Zuberi Msabaha kimeipa pengo tasnia ya habari – Waziri Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mtangazaji maarufu wa kituo cha Radio Free Africa Ndg. Zuberi Msabaha kilichotokea leo alfajiri tarehe 10 Januari, 2018 katika Hospitali ya Uhuru jijini Mwanza.

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa kifo cha Ndg. Msabaha kimeipa pengo tasnia ya habari na hasa katika nyanja ya burudani ambayo marehemu alikuwa mahiri na mburudishaji wa aina yake.

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, uongozi wa kampuni ya Sahara Media Group Ltd, ndugu, jamaa, marafiki na wanahabari wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Kipindi cha uhai wake marehemu Ndg. Msabaha alifanya kazi na kampuni ya Sahara Media Group Ltd kama mtangazaji wa vipindi vya burudani kwenye Redio Free Africa na Star Tv.

Marehemu Msabaha atakumbukwa sana kwa kipindi chake maarufu cha muziki wa dansi cha Bolingo Time cha Radio Free Africa.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa leo Mabatini jijini Mwanza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW