Burudani

Kifo ni ahadi, lazima aliyeitoa aitimize – Nikki Mbishi  

Msanii Nikki Mbishi ameamua kutenga muda wake na kuandika ujumbe au maono ya kile anachokiamini yeye katika maisha ya hapa duniani, na hata baada ya kuodoka katika uso wa dunia.

Nikki Mbishi

“Utajiri wa mali za duniani ni fahari za kupita tu, tajiri alipata nafasi ya kumiliki kila aina ya kitu kimfanyacho afurahie maisha yake. Maskini naye hufurahi kwa hali yake maana ndio majaaliwa ya Mungu wake kwake. Tajiri na maskini hawakupata na hawatopata nafasi ya kujiandalia makazi yao ya milele licha ya kuwa ni dhahiri watakwenda na kuacha milki zao zote aidha za kimaskini au kitajiri.

“Eeeh Mungu wangu nijaalie mwisho mwema maana mimi ni mpofu sijui nukta wala sekunde ya wewe kuchukua kilicho chako toka kwangu. Wanadamu wenzangu kifo ni ahadi na ni lazima aliyeitoa aitimize, tusiishi kama hakuna kesho, tusameheane, tupendane na tujaliane maana gharama ya msamaha, upendo na kujali ni ndogo kuliko gharama ya chuki,visasi na masengenyo,” Nikki ameongeza.

“Binafsi naiwaza siku yangu japo siijui,mimi si mwema hata kidogo mbele za Mungu wangu ila kwa huruma yake napumua si kwamba waliotangulia si wema. Jiandae ile siku yaja, tutalilia nafsi za wengine lakini haitokuwa na maumivu makubwa kama kila mmoja kuililia nafsi yake,” ameandika Nikki Mbishi.

 

By Peter Akaro

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents