Kifungo changu funzo kwa wasanii

Kifungo changu funzo kwa wasanii
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Mohamed ‘TID’, amesema
kuwa kuhukumiwa kwake kifungo cha mwaka mmoja jela ni fundisho tosha
kwa wasanii wa hapa nchini.

TID aliseyasema hayo juzi katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ITV, kuwa baada ya kutumikia kifungo kwa zaidi ya miezi mitano na kupata msamaha, amejifunza mambo mengi sana, pia ni fundisho kwa jamii kwani wengi wanafikiri kuwa kuwa maarufu huwezi kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema kuwa katika kipindi hicho anachokiita cha urekebishaji ameweza kujifunza mambo mengi na kufahamu kuwa hakuna mtu anayeweza kuwa juu ya sheria na kuwataka Watanzania kufanya mambo yaliyo mema.

TID alisema kuwa anawaomba radhi mashabiki wote aliwakosea kwa namna moja au nyingine pamoja na familia ya Ben Mashiba, ambapo alimpiga wakiwa katika sehemu ya starehe.

TID ambaye anamiliki bendi ya muziki huo ya Top Bend imekamilisha albamu inayokwenda kwa jina la Prison Voice inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents