Burudani

Kigezo cha maadili kinatubana kufanya filamu bora – Richie

Muigizaji wa filamu, Single ‘Richie’ Mtambalike, amesema kuendekezwa kwa maadili kupitiliza ndicho chanzo cha kushindwa kuigiza filamu bora zaidi.

12783938_556222947871769_1420792168_n

Richie ,ambaye siku chache zilizopita alishinda tuzo ya filamu bora ya Kiswahili kwenye AMVCA 2016 zilizotolewa Nigeria, mesema wanashindwa kuigiza uhalisia wa kinachotokea kwenye jamii kwasababu serikali imeshikilia maadili sana.

Akizungumza na kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Richie amefafanua kuwa kuna maneno ambayo kiuhalisia yanatumika mtaani hasa kwenye sehemu za vurugu au magenge ya wahuni,lakini ukiyatumia kwenye filamu katika scene zinazohusu maeneo kama hayo filamu hiyo haitaruhusiwa kutolewa kwa kisingizio haina maadili.

Amelalamikia issue hiyo akisema inafanya wao kushindwa kushindana kimataifa kwasababu nchi nyingine wameruhusiwa kufanya hivyo.

Ametolea mfano wa filamu maarufu nchini Kenya ‘NAIROBI HALF LIFE”ambayo ilitumia maneno halisi kulingana na sehemu husika na ikaitangaza Kenya kote duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents