Michezo

Kigi afunga pazia la usajili Singida United, wajigamba kuwa na kikosi bora VPL

Klabu ya Singida United imefunga pazia la usajili baada ya kukamilisha usajili wa winga wa Ndanda FC, Kigi Makasi aliyehudumu kwa nyakati tofauti timu ya Taifa ya Tanzania, Simba S.C na baadae Ndanda Fc.

Kigi aliamua kuivia beji ya ukepteni wa Ndanda Fc na kuelekea katikati mwa nchi ya Tanzania kuungana na timu ya Ushindi ya Singida United.

Wiki iliyopita uongozi wa klabu hiyo ilijinadi kuwa timu hiyo itapambana kufa na kupona kuhakikisha inachukua ubingwa wa ligi msimu wa 2017/18 kutoka na ubora wa kikosi chao.

Taarifa ya Singida United…

Kigi Makasi amekuwa ndio mchezaji anayefunga ukurusa wa usajili ndani ya Singida United kwa msimu wa 2017/2018.

Tulishamaliza kufunga Ukurasa wa wachezaji wanje(7players).
1.Elisha Muroiwa(Zimbabwe)
2.Twafadzwa Kutinyu (Zimbabwe)
3.Simbarashe Nhivi (Zimbabwe)
4.Wisdom Mtasa (Zimbabwe)
5.Shafik Batambuze(Uganda)
6.Dany Usengimana( Rwanda)
7.Michel Rusheshangoga(Rwanda)

Leo tumemaliza kusajili wachezaji wa ndani(9 players).
1.Atupele Green (Jk Ruvu)
2.Miraj Adam (Africa Lyion)
3.Kenny Ally (Mbeya City)
4.Roland Msonjo(Mshikamano Fc)
5.Pastory Athans (Simba)
6.Deus Kaseke(Yanga)
7.Ally Mustapha (Yanga)
8.Salum Chuku (Toto Africa)
9.Kigi Makasi (Ndanda Fc).

Kwa taarifa yako, Kwa sasa Singida United ina jumla ya wachezaji 25.
Wachezaji 16 wamesajiliwa kutoka timu mbalimbali.

Wachezaji 9 ni wale waliosalia baada ya timu kupanda kucheza Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018.

Tunawashukuru vilabu mbalimbali ambao tulifikia makubaliano nao na wamewachukua baadhi ya wachezaji wetu walioipandisha timu, na baadhi ya wachezaji waliomba kuondoka kwa ridhaa yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents