Habari

Kigoma All Stars kuwa kampuni


Lile kundi la mastaa wote wenye asili ya mkoa wa Kigoma All Stars, halitaishia kufanya muziki tu, bali hivi karibuni litakuwa kampuni.
Taarifa hiyo imetolewa jana na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alipokuwa akizungumza na kituo cha radio cha Clouds Fm.
Amesema kampuni hiyo itajenga kituo cha vijana mkoani Kigoma kwaajili ya kusupport vijana wenye vipaji na ndoto za kufanya muziki na filamu.
“ Sasa hivi tunachokifanya tunashirikiana na mashirika mbalimbali ya kimataifa na mashirika ya ndani, kuweza kuhakikisha kituo hicho kinajengwa na kinakamilika,” alisema.
“Kwahiyo sasa hivi Leka Dutigite kwa maana ya Kigoma All Stars, itakuwa ni kampuni ambayo inaendeshwa na wasanii wenyewe, itamilikiwa na wasanii wenyewe 100 percent na sisi tutaoa kama support tu.”
Kingine amesema hafanyi hivyo kwa mkoa wa Kigoma tu kwani tayari ameanza kufanya mazungumzo na wassnii wa Tanga kufanya kitu kama hicho na mwisho upo uwezakano wa kuwa na mradi wa Tanzania All Stars.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents