Habari

Kiingilio Redd’s Miss Tanzania 2012 chatajwa

By  | 

Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kufanyika kwa fainali ya shindano la Redds Miss Tanzania 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, November 3.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International inayoratibu shindano hilo, Hashim Lundenga, alisema mpaka kufikia sasa maandalizi yote yamekamilika na kila kitu kipo tayari.

Katika upande wa burudani, wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Winfrida Josephat ‘Rachel’ na Wanne Star Ngoma Troupe wanatarajiwa kupamba fainali hizo.

Alisema tiketi zimeanza kuuzwa leo, kwenye vituo vilivyopendekezwa kulingana na maoni ya wadau ambapo tiketi moja inauzwa kwa shilingi laki moja.

Maeneo ambayo tiketi hizo zinauzwa ni pamoja na Regency Park Hotel, Rose Garden Mikocheni, Shear Illusions Mlimani City, Ubungo Plaza na Ofisi za Lino Agency Mikocheni.

Lundenga aliongeza kuwa kutokana na ukubwa wa shindano hilo kwa mwaka huu, wale wote watakaofanikiwa kuingia ukumbini, watakaa viti maalumu vilivyowekwa katika hadhi ya kimataifa.

Lundenga alitoa shukrani kwa wadhamini wa shindano hilo, Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original, Star TV na Giraffe Hotel.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments