Habari

Kijana aliyeokota milioni 38 apongezwa na polisi kwa kuzirudisha

Polisi nchini Ujerumani katika mji wa Berlin wamempongeza kijana wa miaka 16 aliyerudisha pochi yenye kitita cha Euro 14,000 sawa na milioni 38 za kitanzania.

Kijana huyo raia wa Iraq ambaye ni mkimbizi aliokota pochi hiyo iliochwa ndani ya treni mjini Berlin na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 79 siku ya ijumaa ya wiki iliyopita wakati akirudi kutoka shule .

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Sabah taarifa zinaeleza kuwa bibi huyo alitoa taarifa kwenye kituo cha polisi na kwa wahudumu wa treni hizo muda mfupi baada ya kusahau pochi yake.

Wazazi wa msichana huyo walidai mtoto wao alikuja na pochi hiyo ikiwa na fedha kiasi cha Euro 14000 lakini baada ya kusikia taarifa kutoka polisi waliamua kurudisha pochi hiyo.

Mnamo septemba 15 mwaka huu tulipokea taarifa kutoka kwa mwanamke mmoja akidai kusahau pochi yake kwenye treni za U-Bahn na leo (jana jumanne) tumeipata pochi hiyo kutoka kwa kijana muaminifu na muhusika tayari ameipata na amefurahi sana,“imeeleza taarifa kutoka kwa polisi wa mjini Berlin na kuthibitisha pia kupitia mtandao wa Twitter.

Kwa sheria za Ujerumani zawadi anayopaswa kupewa mtu yeyote aliyeokota kitu ama pesa ya mtu hupewa asilimia 3 ya thamani yake. Hivyo kulingana na sheria hiyo familia ya mtoto huyo inaweza kupata zawadi ya hadi Euro 350.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents