Habari

Kijana wa Mali aliyemuokoa mtoto ghorofani akutana na Rais, apewa uraia na kazi serikalini

Kijana raia wa nchini Mali, Mamoudou Gassam (22) ambaye Jumamosi iliyopita amefanya kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto mdogo ambaye alitaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne, amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kupatiwa zawadi nzito.


Mamoudou Gassam akiwa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Mamoudou amekutana na Rais Macron mapema Jumatatu hii kwenye Ikulu ya Elysee Palace kwa ajili ya kufanya mazungumzo pamoja na kupongezwa kwa msaada alioutoa.

Rais Macron amempatia cheti cha Uraia wa Ufaransa kijana huyo ambaye alihamia nchini hapo kwa njia zisizokuwa za kihalali takribani miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kutafuta maisha.


Mamoudou akiwa ameshikilia cheti chake cha Uraia wa Ufaransa

Lakini pia Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika jeshi la zima moto la Ufaransa.

Kupitia mtandao wa Twitter Rais Macron ameweka picha akiwa Ikulu na kijana Mamoudou na kuandika, “With Mr. GASSAMA who saved Saturday the life of a child climbing 4 floors with bare hands. I announced to him that in recognition of this heroic act he would be regularized as soon as possible, and that the brigade of the firemen of Paris was ready to receive it.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents