Habari

Kijana wa Marekani aliyekuwa mikononi mwa Korea Kaskazini afariki dunia

Mwanafunzi wa Marekani Otto Warmbier aliyekuwa akishikiliwa nchini Korea Kaskazini kwa takrtiban miezi 15 amefariki dunia wiki moja baada ya kuachiliwa.


Otto Warmbier akiwa mikononi mwa maofisa wa Korea Kaskazini enzi za uhai wake

Familia ya Warmbier ambaye alikuwa na umri wa miaka 22, imesema marehemu amefariki kutokana na unyanyasaji mkubwa aliokuwa akiupata kutoka kwa watu wa usalama wa taifa hilo waliokuwa wakimshikilia.

“When Otto returned to Cincinnati late on June 13 he was unable to speak, unable to see and unable to react to verbal commands. He looked very uncomfortable — almost anguished. Although we would never hear his voice again, within a day the countenance of his face changed — he was at peace. He was home and we believe he could sense that” imesema taarifa iliyotolewa na familia hiyo.


Marehemu Otto Warmbier akiiwa amebebwa kupelekwa hospitali wiki iliyopita

Otto alilazwa katika hospitali moja iliyopo karibu na nyumbani kwake, Cincinnati tangu alipoachiliwa Jumapili ya wiki iliyopita. Madaktari waliokuwa wakimhudumia marehemu wamesema kijana huyo alikuwa na majeraha makubwa ya kuumia neva.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents