Habari

Kijana wa miaka 21, abuni zaidi ya ‘Emojis’ 350 zenye asili na utamaduni wa Kiafrika 

Kutana na O’Plerou Grebet, ambaye amebuni zaidi ya ’emojis’ 350 zenye asili na tamaduni ya Kiafrika ambazo mtu anaweza kuzipakuwa ‘downloadable’ na kuamua kutumia.

O’Plerou Grebet mwenye umri wa miaka 21, kutokea nchini Ivory Coast ni mwanafunzi ambaye anasomea ‘3D design and virtual reality’ ili kumwezesha kupata njia nzuri zaidi katika kazi yake hasa kutambulisha heshima ya Mwafrika na tamaduni zake.

Kijana huyo amezipatia jina ’emojis’ hizo kama ‘Zouzoukwa African emojis’, kwa wale wanaotumia simu janja za Smartphone, kompyuta na baadhi ya vifaa vingine vya aina hiyo basi si wageni katika kukutana na ’emojis’ na pengine hata kuzitumia ambazo huwa zinatoa tafsri ya kitu ama jambo fulani.

Grebet amesema ‘’Jina langu ni O’Plerou Grebet nina umri wa miaka 21, mimi ndiyo mvumbuzi wa Zouzoukwa African emojis,’’ amesema kijana huyo.

O’Plerou Grebet ameongeza ”Wazo langu lilikuwa ni kubuni ’emojis’ ambazo zitakuwa zina endana na tamaduni za Afrika.

 

BY  HAMZA  FUMO

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents