Bongo Movie

Kijiweni Production yatoa neno baada ya ushindi wa T-Junction

Kampuni ya Kijiweni Production inayohusika kutengeneza filamu mbalimbali ikiwemo ya T-Junction imetoa neno lake baada ya kunyakua tuzo za Zimbabwe International Films Festival(ZIFF) kwa ushirikiano na International Image Films Festival(IIFF).

Akiongea na Bongo5, Mtayarishaji na muongozaji wa Filamu hiyo Amil Shivji, amesema kuwa walichaguliwa katika tuzo hizo kubwa za filamu ila kutoana na sababu ziliokuwepo walishindwa kwenda team nzima hivyo walikuwa na mwakilishi kutokea huko.

“Bahati mbaya hatukwenda Zimbabwe kwenye Film Festival, kwa sababu sisi wote hapa tulikuwa busy hapa Dar es salaam katika promotion za T-Junction hatujaweza kwenda lakini kuna rafiki yetu ni Mzimbabwe anaitwa Angeline yeye ndiye aliyekwenda  kupokea na asema tumeshinda tuzo ya Best African Future, hapo kwenye Internation Images Films Festival ambao wamefanya collaboration na Zimbawe International Films Festival,” amesema Shivji.

Pia akaongeza ” Katika tamasha hilo zilionyeshwa filamu 400 kutoka nchi 33 barani Afrika, pia filamu ye ‘Aisha’ iliyotoka mwaka jana iliwahi kuonyeshwa katika tamasha hilo na ilifanikiwa kushinda tuzo ya ‘Best Audience Awards’.

Akasisitiza ” Kwa sasa hivi tuna mipango mingi kuhusu T-Junction tunatuma kwenye Films Festivals zote ndani ya Afrika na nje ya Afrika, tunataka filamu kutoka Tanzania itambulika kwa sababu filamu hii ni nzuri na ina Internatinal standard na stori yake ni nzuri na tumesha ipeleka katika Festivals kubwa na tuna subiria kama imeingia .”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents