Burudani

Kiki za mapenzi kwa wasanii zamchefua Nemo, ‘… uwezo wako ni mdogo’

Msanii muziki Bongo, Nemo amesema haamini msanii kutumia kiki katika mahusiano ndio njia ya kufanya vizuri.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kipotabo’ amefunguka na kueleza kuwa kufanya muziki mzuri ndio njia pekee ya kuliteka soko.

“Achana na kusema kwamba kutoka na fulani ndio kiki nzuri, muziki wako unaofanya ndio utakuwa kiki yako, kwa hiyo mimi sifanyi muziki kwa kutengemea kiki kwa sababu kama unatengemea ina maana uwezo wako ni mdogo katika kazi ya muziki,” Nemo ameimbia Bongo5

“Kiki zinajitokeza zenyewe kwa sababu katika yale matukio yako unakuta limejitokeza jambo limevuja linakuja kuwa kiki lakini siyo kwa kutengeneza,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents