Habari

Kikongwe aliyenusurika kifo Vita ya kwanza ya dunia afariki

Mwanaume wa Afrika Kusini aliyedhaniwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 116.

SA's Fredie Blom, one of world's oldest men, passes away

Nyaraka za utambulisho wa Fredie Blom zinaonesha kuwa alizaliwa katika jimbo Eastern Cape mwezi Mei 1904, ingawa hilo halikuwahi kuthibitishwa na rekodi za Guinnes za dunia(Guinness World Records).

Alipokuwa kijana mwenye umri wa balehe, watu wote wa familia yake walikufa kutokana na janga la mafua -Spanish flu, mwaka 1918. Aliishi na kunusurika vita ya kwanza ya dunia pamoja na vita vya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Imatge

Image caption: Nyaraka za utambulisho za Fredie Blom zinaonesha alizaliwa tarehe 8 Mei, 1904

Bwana Blom ambaye alikua mvutaji wa sigara, aliiambia BBC mwaka 2018 kwamba hakuna siri maalumu ya kuishi maisha marefu.

“Kuna kitu kimoja tu-ni mwanaume aliye juu (Mungu). Ana mamlaka yote. Sina chochote. Ninaweza kufa wakati wowote lakini bado amenishikilia,”

Bwana Blom aliishi maisha ya kufanya kazi za kawaida – ikiwemo kazi ya kilimo katika shamba na baadae katika kiwanda cha ujenzi – alistaafu akiwa na umri wa miaka themanini zaidi ya 80.

Familia ya Bwana Blom amesema alikufa kifo cha kawaida mjini Cape Town Jumamosi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents