Michezo

Kikosi cha Simba kutua Dar kibabe

Kikosi cha klabu ya Simba kinatarajia kurejea kikitokea nchini Djibouti katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Simba SC ilikuwa nchini humo kwaajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF dhidi ya Gendarmerie na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1 – 0 bao likifungwa na mshambuliaji wao raia wa Uganda, Emmanuel Okwi katika kipindi cha pili.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo umeseme kuwa Simba itaondoka Djibouti majira ya saa 12:05 jioni.

Kikosi cha Simba kurejea leo nchini.
Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini Djibouti saa 12:05 jioni ya leo kurejea nchini kwa kutumia usafiri wa ndege kupitia Shirika la KQ.

Simba SC imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya kuifungashia Gendarmerie kwa jumla ya mabao 5 – 0.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents