Tupo Nawe

Kikosi cha Taifa Stars chatangazwa, wachezaji 10 watoka nje ya Tanzania, wapo wa Hispani, Ubelgiji, Botswana na Misri ni kufa au kupona dhidi ya Uganda

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Emmanuel Amunike leo ametaja kikosi cha wachezaji 25 watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu Fainali za Afrika AFCON2019 zitakazofanyika mwaka huu nchini Misri.

Mchezo huo ni dhidi ya Uganda utakaopigwa nchini Tanzania Machi 24 mwaka huu ambapo kwa Tanzania ushindi ni lazima ili kufuzu fainali hizo ikitegemea pia matokeo ya mchezo kati ya Cape Verde dhidi Lesotho ambazo ziko kundi moja.

Kikosi kilichotajwa leo kimejumuisha wachezaji wanne kutoka Yanga, watatu kutoka Simba, wawili kutoka Azam FC, wawili kutoka Mbao FC, kumi kutoka nje ya Tanzania na wanne kutoka vilabu mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.

Kikosi chenyewe hiki hapa.

Kutoka Yanga. 
1. Feisal Salum. 
2. Gadiel Michael. 
3. Kelvin Yondan. 
4. Andrew Vicent.

Kutoka Simba. 
1. Aishi Manula. 
2. Jonas Mkude. 
3. John Bocco.

Kutoka Azam FC. 
1. Mudathir Yahya. 
2. Agrey Moris.

Kutoka Mbao FC. 
1. Metacha Mnata.
2. Vicent Philipo.

Wengine kutoka timu za ndani ya Tanzania. 
1. Aron Kalambo – TZ Prisons. 
2. Suleiman Salula – Malindi FC ya Zanzibar. 
3. Ally Mtoni – Lipuli FC. 
4. Kennedy Wilson – Singida United.

Wanaocheza soka nje ya Tanzania. 
1. Hassan Kessy – Nkana FC ya Zambia. 
2. Yahya Zayd – Ismaily ya Misri. 
3. Himid Mao – Petrojet ya Misri. 
4. Shiza Kichuya – ENPPI SC ya Misri. 
5. Saimon Msuva – Difaa El Jadid ya Morocco. 
6. Rashid Mandawa – BDF XI ya Botswana.
7. Thomas Ulimwengu – JS saoura ya Algeria. 
8. Shabani Idd – Tenerife ya Hispania. 
9. Farid Musa – Tenerife ya Hispania.
10. Mbwana Samatta – KRC Genk ya Ubelgiji

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW