Kikosi kipya cha polisi chaundwa Nigeria

Kiosi maalumu cha kupambana na wizi Special Anti-Robbery Squad -kilishutumiwa kwa ukatili

Mkuu wa polisi nchini Nigeria amesema kikosi kipya kimeundwa ili kuchukua nafasi ya kikosi tata maalumu cha polisi cha kukabiliana na wizi kinachofahamika Sars, ambacho kilivunjwa kufuatia maandamano ya ukiukaji wa haki za binadamu dhidi yake.

Kikosi kipya kitajulikana kama Swat au kikosi maalumu cha cha silaha na mbinu – (Special Weapons and Tactics Team).

Waandishi wa habari wanasema Wanigeria wengi hawana Imani na wanaendelea kuandamana wakitaka yafanyike mageuzi makubwa katika polisi ya nchi hiyo.

Katika juhudi za kutatua kuondoa hofu miongoni mwa Wanigeria mkuu wa polisi amesema kuwa polisi wote kutoka katika kikosi kilichovunjwa watapitia uchunguzi wa kisaikolojia na kimatibabu kabla ya kupata mafunzo zaidi na kupelekwa tena katika sehemu za kazi.

Pia aliagiza kuachiliwa huru bila masharti yoyote kwa watu wote waliokamatwa wakati wa maandamano.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW