Habari

Kikosi watangaza vita dhidi ya mauaji ya Albino

kikosi watangaza vita dhidi ya mauaji ya Albino
Wasanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, wameamua kutumia sanaa ya muziki huo kutangaza rasmi, tamko la vita dhidi ya watu wanaosababisha na wanaofanya mauaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanaojulika kama Albino. Tamko hili linatambulisha kauli mbiu isemayo ” HIP-HOP AGAINST ALBINO VIOLENCE” inayomaanisha kwamba wasanii hao wameamua kupambana na ukatili unaofanywa dhidi ya maalbino.

Umoja huu wa wasanii Hip-Hop unaoongozwa na kundi la Kikosi cha Mizinga ambao ndiyo waratibu umeamua kufanya hivi kwa sababu wao ni wanaharakati wanaoangalia matatizo yaliyopo kwenye jamii yetu ya Kitanzania.
Pili wameamua kuungana na serikali na asasi nyingine zote zilizo mstari wa mbele katika vita hii dhidi ya watu washirikina na wakatili waliojitokeza kwenye nchi yetu. Muungano huu wa wasanii umesharekodi nyimbo inayopinga mauaji hayo na imeanza kusambazwa rasmi leo tarehe 9.03.2009. Vile vile wasanii hao watasambaza video ya nyimbo hiyo siku chache zijazo kwenye vituo vya luninga nchini.

 

Kuhusu wimbo huo unaoitwa ” HIP-HOP AGAINST ALBINO VIOLENCE” umewashirikisha wasanii kutoka Kikosi cha Mizinga akiwemo Kalapinna, Sumalago, Mau na Gwalu Fukuda, Nduli anayetokea serious Manizo, Coin Moko tokea Vinara, Hasani wa United, Ibony Moalim, Zimwi na Half Animal. Wimbo huo upo katika lugha mbili, ambazo ni kiswahili na Kingereza. Wasanii hawa wameamua kutumia sanaa ya muziki wa Hip-Hop katika kuelimisha ma kurekebisha jamii dhidi ya mauaji ya ndugu zetu, jamii zetu na marafiki zetu, Albino.

 

Wasanii hawa wanaomba ushirikiano kwa vyombo vyote vya habari bila kujali tofauti kwa sababu hili ni suala la kitaifa zaidi na wanatengemea support kubwa kurekebisha na kuelimisha jamii. Vile vile umoja huu uliwasihi wasanii waribu kutumia sanaa zao katika kuisaidia jamii ili iondokane na ujinga na dhana potofu kama ya mauaji ya albino kwa ajili ya utajiri.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents