Siasa

Kikwete aipa Big Up Vodacom

Rais wa jamuhuri ya muungan wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ushiriki wake mzuri wa kuhudhuria mkutano wa nane wa Sullivan unaoendelea jijini hapa.

jk.jpg

Rais wa jamuhuri ya muungan wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ushiriki wake mzuri wa kuhudhuria mkutano wa nane wa Sullivan unaoendelea jijini hapa.

 “Ninawapongeza Vodacom Tanzania kwa ushiriki wao katika mkutano huu kwani imeonesha ni namna gani inaweza kuwa na ushirikiano waliouonesha katika hili” alisema Rais Kikwete.

Aliendelea kusema “ushiriki wa sekta binafsi katika mkutano huo ni wenye manufaa na mchango mkubwa na kwamba sekta hiyo ina nafasi kubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu” Naye Hope Masters, Mtendaji Mkuu na Rais wa Taasisi ya Sullivan, aliipongeza Vodacom Tanzania kwa namna ya pekee kutokana na ushiriki wake katika mkutano huo na kwamba Vodacom ni moja wa wadau waliochangia mafanikio ya mkutano huo.

“Naipongeza Vodacom Tanzania kwa ushiriki wake wa karibu ambao umeweza kufanikisha mkutano huu” alisema. Vodacom Tanzania ndiyo mtandao rasmi wa mawasiliano katika mkutano huo ambao ulifunguliwa juzi usiku na Rais Kikwete.

Mbali na kuwa mtandao rasmi wa mawasiliano pia Vodacom imetengeneza kituo maalum cha mawasiliano ambacho kinatumiwa na Waandishi wa Habari kutoka katika sehemu mbalimbali za Dunia wakati wakiripoti matukio ya mkutano huo mkubwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare, alisema kwamba Vodacom Tanzania inajisikia faraja kufanya biashara zake katika Tanzania kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo amani, utulivu na ukuaji endelevu wa uchumi.

Alisema kwa kutambua kwamba Tanzania ni nchi inayoendelea na inayokabiliwa na changamoto katika ukuaji wa sekta mbalimbali ikiwamo mawasiliano, Vodacom Tanzania imekuwa ikiwekeza ili kuhakikisha kwamba maendeleo ya watu yanapatikana kwa kuwawezesha watu kuwasiliana bila vikwazo.

Alisema idadi ya wateja hai wa Vodacom Tanzania wamekuwa wakiongezeka kila mwaka, hivi sasa Vodacom ina wateja hai zaidi ya milioni nne huku ikitoa ajira za moja kwa moja na zile ambazo si za moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 50,000.

Mkurugenzi huyo alisema Vodacom Tanzania imekua ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii lengo likiwa ni kuboresha maisha ya Watanzania, maeneo ambayo ina jihusisha moja kwa moja ni utengenezaji wa ajira, uibuaji wa vipaji vya michezo kwa vijana, pamoja na utoaji wa huduma mablimbali za kijamii kupitia Taasisi yake ya Vodacom Foundation.

Mkutano huo unahuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 4,000 pamoja na watu mbalimbali mashuhuri akiwamo Rais mstaafu wa Nigeria , Olesugem Obasanjo, Mchungaji Jesse Jackson na Balozi Andrew Young.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents