Siasa

Kikwete aombwa kuingilia wanafunzi Ukraine

WAZAZI wa wanafunzi 29 wa Tanzania waliojisalimisha katika ubalozi wa Uingereza nchini Ukraine, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete, kuingilia kati suala la watoto wao na kuwachukulia hatua maafisa wa Wizara ya Sayansi, Teknknolojia na Elimu ya Juu, waliowakana wanafunzi hao.



Na Abdallah Bawazir


WAZAZI wa wanafunzi 29 wa Tanzania waliojisalimisha katika ubalozi wa Uingereza nchini Ukraine, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete, kuingilia kati suala la watoto wao na kuwachukulia hatua maafisa wa Wizara ya Sayansi, Teknknolojia na Elimu ya Juu, waliowakana wanafunzi hao.


Wakizungumza muda mfupi baada ya kikao chao kilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, kujadili matatizo yaliyowapata watoto wao, wazazi hao, huku wakiwa na wasiwasi juu ya maisha ya watoto wao ugenini, walisema wameshangazwa na hatua yawizara hiyo kuwakana wanafunzi hao, wakati waliondoka nchini kwa baraka zote za wizara na ahadi kuwa watalipiwa masomo yao.


Mmoja wa wazazi hao, Sheikh Waziri Omar Nyello, akizungumza kwa niaba ya wenzake, alimuomba Rais Kikwete, awaokoe vijana hao kwani walikwenda Ukraine kwa ajili ya masomo kwa idhini ya Serikali.


Alisema kabla ya kuondoka nchini, vijana hao walifuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na kuomba mikopo kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kukubaliwa.


Sheikh Wazir alifafanua kuwa wanafunzi hao walikwenda Ukraine Septemba mwaka jana baada ya kukubaliwa kupewa mikopo na Bodi ya Mikopo kwa ajili ya kuanzia muhula wa masomo wa 2005/06 lakini kutoka na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wao, walishindwa kwenda Ukraine mwaka huo na kuomba mikopo hiyo waanze kupewa muhula wa masomo wa 2006/07.


Walisema kabla ya wanafunzi hao kuondoka, walikubaliana na Bodi ya Mikopo pamoja na Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kuwa mikopo yao itaanza kutolewa muhula huo wa 2006/07.


Sheikh Waziri alisema kabla ya kuondoka nchini wanafunzi hao walipewa sharti la kujinunulia wenyewe tiketi za ndege na kuahidiwa kuwa fedha zao za mikopo zitatumwa wakishafika huko.


“Tunahisi maafisa wa Wizara ya Elimu ya Juu na Bodi kabla ya kubalisha vigezo walisahau kuwa kuna wanafunzi wapo Ukraine na waliokubaliwa mikopo kwa vigezo vya zamani, sasa walipobaini wamefanya makosa wakaamua kuwageuzia kibao kuwa serikali haiwatambui ili kulinda kibarua chao,” alisema Sheikh Waziri.


Wakizungumza na Mwananchi toka Kiev, wanafunzi hao walisema Mwananchi kuwa walijisalimisha katika ubalozi wa Uingereza uliopo Kiev baada ya vyuo wanavyosoma kuwataka wawe wameondoka kufikia Jumatatu iliyopita na wawe wamelipa ada ama sivyo watakamatwa na kupelekwa polisi.


Pia walilalamika kuwa baada ya Serikali kushindwa kuwatumia fedha za ada pamoja na za mahitaji muhimu, wamekuwa wakiishi maisha ya mateso bila ya chakula huku, usalama wa maisha yao ukiwa hatarini.


Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents