Siasa

Kikwete Kutoingilia Mashitaka Epa

RAIS Jakaya Kikwete amesisitiza  kuwa katu hataingilia suala la matatizo ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na watuhumiwa wa Fedha hizo kwani mzigo huo uko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP.

 

RAIS Jakaya Kikwete amesisitiza tena kuwa katu hataingilia suala la matatizo ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na watuhumiwa wa Fedha hizo kwani mzigo huo uko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP.

Kikwete alisema kuwa dhamira ya serikali siyo kuruhusu wanasiasa kutumia suala la watuhumiwa EPA kupigana vita wenyewe kwa wenyewe, bali ni kuongozwa na utawala wa kisheria na kuwa DPP ndiye mwenye madaraka na mamlaka kikatiba hivyo hatomwingilia.

Rais Kiwete alitoa kauli hiyo jana mjini Arusha alipokutana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya Shirika la Fedha Duniani (IMF), Antoinette Sayeh kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC baada ya kufungua mkutano wa 14 wa vyombo vya fedha.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango ya Uchumi, Mustafa Mkullo, Katibu Mkuu wa Wizara wake Gray Mgonja, Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndullu na gavana wasaidizi.

“Dhamira yetu sasa ni kuongozwa na utawala wa kisheria, na siyo kuruhusu wanasiasa kutumia EPA kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.”

“Sasa kila kila kitu kiko mikononi mwa DPP, mwisho wa siku yeye ndiye mwenye madaraka na mamlaka ya mwisho kisheria. Mamlaka yake ni ya kikatiba, wala haliwezi kuwa suala la uamuzi wa kisiasa. Kamwe hata mimi siwezi kumwingilia,” ilisema sehemu ya taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, kwa vyombo vya habari.

Kikwete alisema serikali imefanya kila linalowezekana kuhusu EPA mbali na kuwa madeni hayo ni ya muda mrefu zaidi ya miaka 30 iliyopita na kwamba hatua za kisheria.

“Tumefanya kila linalowezekana kuhusu EPA. Kumbuka haya ni madeni ya karibu miaka 30 iliyopita. Lakini sasa tumefikia kwenye hatua za kisheria,” alisema Rais Kikwete

Alisema serikali imejifunza mengi kuhusu mifumo ya udhibiti na kwamba lililo muhimu ni kuhakikisha suala kama la EPA halirudiwi tena.

“Tumejifunza mengi kuhusu mifumo yetu ya udhibiti na muhimu hapa ni kuhakikisha kuwa jambo kama hili halirudiwi tena,” alisema Kikwete.

Akizungumzia mageuzi ya uchumi Rais Kikwete alisema kuwa Tanzania kamwe haitarudi nyuma wala kuacha mageuzi yake ya sasa ya kiuchumi ambayo yameleta manufaa makubwa kwa wananchi.

Alisema serikali itaendeleza mageuzi hayo ingawa kumekuwepo na kelele za baadhi ya wanasiasa kupinga mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea kufanyika nchini na mchango wa sekta binafsi katika uchumi.

Kikwete alisema kelele hizo za baadhi ya wanasiasa ni ushahidi dhahiri kuwa wanasiasa hao wamesahau hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwa inaikabili nchi kabla ya kuanzishwa kwa mageuzi ya sasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents