Siasa

Kikwete, Mbeki waondoa viza

Marais Jakaya Kikwete wa Tanzania na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini wanakutana leo jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, watashuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kuondoa viza kwa watumisi wa serikali na shughuli za kidiplomasia.

Na Apolinary Kweka



Marais Jakaya Kikwete wa Tanzania na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini wanakutana leo jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, watashuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kuondoa viza kwa watumisi wa serikali na shughuli za kidiplomasia.


Akizungumza kuhusu mkutano huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Bw. Basil Mramba aliwaeleza waandishi wa habari kuwa wakuu hao watajadili ushirikiano zaidi wa kiuchumi na kibiashara baina ya nchi hizo.


Alisema katika mkutano huo, Mawaziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hizo, watatiliana saini makubaliano ya kuondoa viza kwa watumishi wa serikali na za kidiplomasia ili waweze kwenda katika nchi hizo bila kuwa na viza.


Alisema tayari kuna mkataba wa kulegeza viza baina ya Tanzania na Afrika Mashariki.


Aidha, Waziri Mramba alisema kuwa hatua inayofuatia baada hiyo ni kupeleka makubaliano hayo kwenye Mabunge ya nchi hizo ili yaweze kuridhia.


Mbali na hayo, Bw. Mramba alisema viongozi hao watataoa maamuzi kuhusu maeneo ya ushirikiano hususan katika miradi mbali mbali ya kiuchumi na kibiashara ili nchi husika ziweze kunufaika.


Mbali na utiaji saini makubaliano hayo, viongozi hao pia watahudhuria uzinduzi wa Tume ya Marais ya Uchumi (PEC).


Vile vile, Bw. Mramba alisema hatua hiyo inatokana na Afrika Kusini kuwekeza sana katika viwanda, mahoteli, madini na utalii na hivyo kuliingizia Taifa mabilioni ya fedha.


Alitoa mfano wa mwaka juzi kuwaTanzania iliingiza fedha za kigeni Sh. bilioni 700 kutokana na biashara baina yake na Afrika Kusini wakati Kenya na Uganda zilikuwa ni Sh. bilioni 300.


Tayari mwaka jana, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliridhia kuondoa viza baina ya Tanzania na Msumbiji.


Mkutano huo ulitanguliwa na wa Mawaziri na wataalamu kutoka nchi hizo ambao pamoja na mambo mengine alijadili ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizo.


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents