Kila la Kheri Amanda

Watanzania tumeweza kumpata Miss Universe Tanzania Bi Amanda Sululu ambaye amemrithi Mwanadada Flaviana Matata  aliyewahi kubahatika kufikia mpaka hatua ya kumi bora katika mashindano kama hayo…

amanda_2.jpg

 

Watanzania tumeweza kumpata Miss Universe Tanzania Bi Amanda Sululu ambaye amemrithi Mwanadada Flaviana Matata aliyewahi kubahatika kufikia mpaka hatua ya kumi bora katika mashindano kama hayo yaliyowahi fanyika mwaka jana.

Kuchaguliwa kwake kuwa Miss Universe Tanzania kunampa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Universe kinachotarajiwa kufanyika huko Vietnam mnamo July 14 ambapo washiriki zaidi ya 80 kutoka kote duniani wanatarajiwa kuwepo katika kuwania taji hilo.

Kutoka Afrika walioingia hatua hiyo ni Tansey Coetzee kutoka Afrika ya Kusini na warembo kutoka Misri, Ghana, Mauritius na Nigeria hawapo katika orodha hiyo.

Miss Universe Venezuela, Diana Mendoza ameshika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo akifuatiwa na warembo wa Marekani, Puerto Rico, Panama, Trinidad and Tobago, Mexico, Ireland, Australia, Colombia na Thailand.

Kwa namna moja au nyingine hii ni hatua mojawapo ambayo inaipatia sifa nchi yetu pamoja na kuitangaza kwa ujumla…hatuna jinsi zaidi ya kumtakia kila la kheri Mtanzania mwenzetu Amanda Sululu.

 

amanda_1.jpg

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents