Tupo Nawe

Kila mwanaume anatamani kuwa na Vanessa Mdee, Nampenda sana Rotimi – JUX

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, JUX amesema kuwa amefurahi sana kumuona mpenzi wake wa zamani, Vanessa Mdee kupata mchumba mpya, Kwani hali hiyo itamrudisha kwenye furaha.

Jux, Vanessa Mdee na Rotimi

Jux amedai kuwa amekuwa akimuombea Vanessa Mdee apate mchumba mpya ili kupunguza chuki baina yao.

Kuna muda nilikuwa nasubiri sana kuona Vanessa Mdee aje kuwa tena na furaha, Unajua kwenye mapenzi ikitoa mmoja ameachwa kuna mambo huwa hayaendi sawa, Drama na vitu kama hivyo.. Lakini ikitokea wote mpo kwenye mahusiano mnakuwa sawa na mnakuwa na furaha. Nilichokuwa nahitaji ni amani baina yetu, Kwa kweli mimi nafurahi sana naamini kwa sasa anafuraha. By the way nimeangalia tamthiliya ya POWER mara nyingi, Nampenda sana Rotimi jinsi anavyoigiza,“, amesema Jux kwenye mahojiano yake na kituo cha Radio cha Kiss FM.

Kwa upande mwingine, Jux amesema kuwa Vanessa Mdee ni aina ya mwanamke ambayo kila mwanaume angetaka kuwa nae kwani ni mpambanaji na ni mrembo pia hawezi kumzungumzia kwa ubaya.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW