Michezo

Kili Marathon Yazinduliwa

 

Kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro jana jioni ilizindua rasmi mbio za tisa za Kilimanjaro marathon kwa mwaka 2010.

Mbio hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 2011 zilizinduliwa rasmi na mgeni rasmi  katika hafla hiyo,  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Michezo na Utamaduni Professa Hermus Mwansoko .

Akiongea katika uzinduzi huo Prof. Mwansoko alisifu juhudi za TBL kupitia bia ya Kilimanjaro ambapo alisema mashindano hayo yamekuwa chachu ya kuinua vipaji mbali mbali vya mchezo huo pamoja na kuongeza ushindani katika ngazi ya taifa.

Naye meneja wa kinywaji cha bia ya Kilimanjaro ambao ndio wadhamini wakuu wa mbio hizo bwana George Kavishe alisema wao kama kampuni na wadhamini wanajisikia fahari kuendelea na udhamini wa shindano hilo ambalo kwa mwaka huu linaingia mwaka wa 9.

Aidha uzinduzi huo ulishuhudiwa na baadhi ya washiriki wa mashindano hayo kutoka Tanzania pamoja na wanariadhaa wa zamani Suleiman Nyambui ambaye ni katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania na mwanariadha wa zamani Bwana Juma Ikangaa pamoja na wakurugenzi wa makampuni shirikishi ya Executive Solutions na Wild Frontiers bwana Aggrey Marealle na John Addison.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents