Kili Tanzania Music Awards 2009
Hatimaye Kili Tanzania Music Awards zilifikia kilele chake hapo jumamosi ndani ya Diamond Jubilee. Mkurugenzi wa Zizzou Fashion Bw. Tippo ambaye pia ni Meneja wa
mwanamuziki Mangwea alipokea tuzo kwa niaba ya msanii huyu kutoka kwa CEO wa Bongo5 Media
Group, Mangwea
ameshinda tuzo ya masanii bora wa Rap. Bofya hapa kuangalia video kibao.
Msanii kutoka Marekani Howard Bailey ‘Chingy’ alicheza ‘Ngoma Itambae’ kabla ya kumkabidhi tuzo Chidi Beenz kama msanii bora wa Hip Hop.
Kwa upande wa Jahazi Modern Taarab iliyo chini ya Mzee Yusuf walipata tuzo mbili moja ya wimbo bora ya taarab ambayo ni V.I.P na albamu bora ya taarabu ambayo pia ni V.IP.
Matonya alipata tuzo mbili ambazo ni wimbo bora wa kushirikiana uitwao ‘Anita’ na Wimbo bora wa Mwaka ambao pia ni ‘Anita’, ambao alishirikiana na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’.
Wasanii wengine waliotwaa tuzo hizo ni Mwimbaji bora wa Kike iliyochukuliwa na Keysha wa Tip Top Connection, Mwimbaji bora wa Kiume alichukua M.B Doggy, Albamu Bora ya Taarabu ni V.I.P ya kundi la Jahazi.
Wimbo Bora wa Kiswahili (bendi) ni ‘Heshima kwa Mwanamke’ ya FM Academia, Albamu bora ya Kiswahili (bendi) ni Akudo Impact ‘Pekecha Pekecha’.
Orodha nzima ya washindi ni:
1. Mwimbaji Bora wa Kike- Keisha
2. Mwimbaji Bora wa Kiume- Mb Dogg
3. Albamu Bora ya Taarab- VIP(Jahazi Modern Taarab)
4. Wimbo Bora wa Taarab- VIP (Jahazi Modern Taarab)
5. Wimbo Bora wa Mwaka- Anita (Matonya ft Lady JayDee)
6. Wimbo Bora wa Kiswahili- Heshima kwa Mwanamke (FM Academia)
7. Albamu Bora ya Kiswahili- Pekecha Pekecha(Akudo Impact)
8. Wimbo Bora wa R& B- Natamani (Q Jay ft Makamua & Joslin)
9. Albamu Bora ya Muziki Asilia- Dela Dela( Che Mundugwao)
10. Wimbo Bora wa Hip Hop- Ngoma Itambae(Chid Benz)
11. Wimbo Bora wa Reggae- Ripoti (Tunda Man)
12. Msanii Bora wa Rap- Mangwea
13. Wimbo Bora wa Afrika Mashariki- Salary(Nameless from Kenya)
14. Mtunzi Bora wa Muziki- Karama Legesu
15. Mtayarishaji Bora wa Muziki- Hammi B
16. Mwandikaji Bora wa Muziki- Prof.Jay
17. Wimbo Bora wa Zouk- Nalivua Pendo(Mwasiti)
18. Mtayarishaji Bora wa Video- Kallaghe Production
19. Wimbo Bora wa Collaboration- Anita (Matonya ft Lady Jaydee)
20. Wimbo Bora wa Asilia- Kazi ya Dukani(Dogo Mfaume)
Bofya hapa kuangalia video kibao pamoja na tuzo zote….