Shinda na SIM Account

Kilimanjaro Stars yachakazwa na Wazanzibar

Timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars ) imekubali kipigo cha kwanza cha goli 2-1 kwenye Mashindano ya kuwania ubingwa wa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Senior Challenge Cup), dhidi  ya ‘Zanzibar Heroes’.

Mchezo huo uliopigwa kunako uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, Kilimanjaro Stars ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Wazanzibari kunako dakika ya 28 kupitia kwa Himid Mao kabla ya magoli mawili ya ushindi ya Zanzibar Heroes kufungwa kipindi cha pili.

Matokeo mengine ya mechi za leo ni Burundi wameibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Ethiopia na mchezo mwingine unaoendelea kwa sasa ni kati ya Rwanda na Libya.

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW