Burudani

Kilimanjaro waingia BSS

 

Kampuni ya Bia  Tanzania  (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro imeingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Benchmark Production kwa ajili ya kudhamini mashindano ya Bongo Star Seach [BSS] na msimu huu itatumia zaidi ya Sh100 milioni katika  kuboresha mashindano hayo ya kuinua vipaji.

Michuano hiyo ya BSS ambayo taji lake linashikiliwa na Pascal Kasian kutoka Mwanza ambayo ni maalum kwa ajili ya kuibua wasanii wachanga, tangu kuanzishwa kwake huu msimu wa nne na tayari mchakato wake umeanza.

Meneja wa Kilimanjaro, George Kavishe aliliambia Mwananchi jijini jana kuwa kutokana na kampuni hiyo kutambua umuhimu wa wasanii, ndiyo maana imeamua kuunganisha nguvu na Benchimark ili kuwafikisha kilele wasanii kama kauli mbiu ya kampuni yao inavyosema.

‘’Kampuni imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali nchini na ndiyo maana tukaamua kudhamini na hii ya BSS kwa muda wa miaka mitatu na msimu huu tumetenga zaidi milioni 100 katika kufanikisha zoezi hilo.’’ alisema Kavishe.

Mkurugenzi wa Benchimark Production, Rita Paulsen aliwashukuru TBL kwa udhamini huo mkubwa na  kuahidi kuboresha zaidi BSS kuanzia zawadi za washindi pamoja na kuandaa vipindi vizuri vitakavyowafurahisha watazamaji na wapenzi wote wa mashindano hayo.

Aliongeza kuwa msimu huu kumekuwa na mabadiliko katika upande wa majaji kwani kutakuwa na majaji waaalikwa kama ilivyokuwa walipoanza mikoani na sio kama ilivyo miaka ya nyuma.

‘’Majaji wa msimu huu watakuwa ni wa kualikwa tofauti ilivyokuwa miaka iliyopita, anaweza kuwa yeyote ili kila mmoja kutoa ushirikiano na kuona ni jinsi gani mashindano hayo yanavyoendeshwa.’’ alisema Paulsen ambaye alikuwa akisaidiana na Salama Jabir, Master J na Majani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents