Habari

Kim Jong-Un akubali mualiko wa kuzuru Marekani, wapinzani wasema uongozi wa Trump unachochea udikteta duniani

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un amekubali mualiko wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa kuzuru nchini mwake hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini (KCNA) .

Imeelezwa kuwa viongozi hao wawili walipeana mialiko siku ya Jana walipokutana nchini Singapore kwenye mkutano wao wa kwanza na wa kihistoria kwa mataifa hayo mawili.

Kwa mujibu wa KCNA, Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amesema kuwa na yeye pia amemualika Trump kuzuru nchini mwake na kusisitiza kwamba kuna haja ya dharula ya kusitisha hatua za kijeshi za uchochezi zinazokera mataifa hayo mawili.

Moja ya hatua kubwa ni ile ya Majeshi ya Marekani na Korea Kusini kuacha mpangp wao wa kila mwaka wa kufanya mazoezi ya kijeshi.

Hakuna taarifa rasmi ni lini Kim Jong-Un atazuru nchini Marekani. Hatua ya Trum kukutana na Kim imeibua mjadala mkubwa nchini Marekkani hususani kwa Chama cha Democratic ambapo wanadai kuwa uongozi wa Trump unachochea udikteta duniani.

Mpaka sasa Trump ameshafanya mazungumzo ya simu na kuonana na viongozi wakubwa ambao wanaodaiwa na Chama cha Democratic kuongoza kidikteta akiwemo Rais Vladimir Putin.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents