AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Kim Kardashian aunga mkono maandamano

Kim Kardashian ameonekana kuyaunga mkono maandamano ya nchini Armenia.

Mrembo huyo ameonyesha hisia zake hizo kupitia ujumbe ambao ameuandika kwenye mtandao wake wa Instagram huku akifurahishwa na umoja wa wananchi hao kwenye maandamano hayo ya amani ambayo yelidumu kwa siku 11.

Kupitia mtandao huo, Kim ameweka picha hiyo hapo juu na kuandika, “Ni msisimko sana kuona Waarmeni wote wameungana katika maandamano ya amani yaliyoleta utofati. Ni siku ya kihistoria kwa Armenia. ❤️🇦🇲💋 Nimetumia picha hii niliyokuwa huko Armenia kwa sababu mwanamke huyu aliugusa moyo wangu na mimi naheshimu anawakilisha moyo wa Waarmenia wengi wenye nguvu!.”

Maandamano hayo yalifanikiwa kumng’oa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Serzh Sargsyan siku ya Jumatatu hii.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW