Burudani

Kim Kardashian na Kanye West wakataa mamilioni ya fedha kufanya hili

Kim Kardashian na mumewe Kanye West wamedaiwa kukataa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuuza picha za kwanza za mtoto wao wa tatu aliyezaliwa Jumanne hii.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Blog kubwa na majarida mbalimbali yaliomba kupata picha za kwanza za mtoto huyo mwezi mmoja kabla.

Chanzo hiko kimeongeza kuwa, wameambiwa Kim na Kanye hawatafikiria kuchukua pesa kwa picha za kwanza za mtoto huyo kutokana na kufanya hivyo kungevunja maadili yao.

Mtoto huyo anadaiwa kuwa ni wakike. Hapo awali Kim na Kanye walianza kuonyesha picha za watoto wao North na Saint miezi miwili baada ya kuzaliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents