Habari

Kimbuga kingine chaibuka Ufilipino na Hong Kong chasababisha vifo vya watu zaidi ya 30

Kimbuga kingine chaibuka Ufilipino na Hong Kong chasababisha vifo vya watu zaidi ya 30

Takriban watu thelathini wameuawa baada ya kimbunga Mangkhut kupiga kaskazini mwa Ufilipino.Wengi kati yao walikumbwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.Maeneo mengi ya kisiwa cha Luzon yamejaa maji, yakiwemo mashamba ambayo huzalisha mazao makuu nchini humo ya mpunga na mahindi.

Katika eneo hilo kunaelezwa kuwa kuna familia takriban elfu ishirini na sita na mia tatu na sitini na saba zilizoathirika ambazo zinahitaji msaada wa chakula na mahitaji mengine.Afisa wa kutoka shirika la msalaba mwekundu Chris Staines ameiambia BBC kuhusu kuwepo kwa hatari ya maporomoko ya udongo katika maeneo ya milima nchini Ufilipino ambayo yalikumbwa na kimbunga.

”Pepo za mansoon za kusini magharibi zimekwisha, na kusababisha eneo kuwa la maji kabla ya kimbunga cha Mangkhut kupiga, na kusabisha mvua zaidi”.Akizungumza na BBC, mratibu wa shirika la misaada la Umoja wa mataifa nchini Ufilipino, Ola Almgren ameeleza changamoto zinazotakiwa kushughulikiwa na mashirika ya misaada.

”Kimbunga hiki kimesabisha madhara makubwa mawili :upepo wake na maji. Tunasubiri kusiki zaidi katika maeneo mengine ni kwa namna gani yameathirika na mvua ambayo ilibebwa na kimbunga.Hivyo tunachokifanya sasa ni kufanya tathimini kuhusu misaada, na uharibifu.Tunachukua hatua kadiri mazingira yanavyotuhitaji kwa kutumia rasilimali tulizonazo.Tunajiandaa kuongeza jitihada kukabili hali hii tukiwa na rasilimali za kimataifa ambazo zitahitajika”.

Sambamba na kusababisha vifo, kimbunga Mangkhut kimeleta hasara ya mabilioni ya dola katika nchi za Ufilipino na Hong Kong.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents