Tupo Nawe

Kimbunga Amphan chaipiga India na Bangladesh, 22 wafariki

Kimbunga kikali kimeikumba India na Bangladesh, na kusababisha madhara makubwa hii leo Alkhamisi. Taarifa zinaelezea kwamba watu wasiopungua 22 wamefariki.

Zyklon Amphan (AFP/NASA Earth Observatory)

Mamlaka za hali ya hewa nchini India zinasema Kimbunga Amphan kilianzia kwenye Ghuba ya Bengali nje kidogo ya pwani ya mashariki ya India. Baadae kimbunga Amphan (um-pun) kilielekea kaskazini kwenye pwani ya mashariki ya India na Bangladesh.

Kimbunga hicho ambacho ni kikali zaidi kuwahi kutokea kwenye pwani ya India mnamo karne hii ya ishirini na moja, kimeipiga miji ya Tala na Buri Goalini huko Bangladesh na Culcutta, India kikiwauwa watu kadhaa na kuharibu miundombinu. Kiwango kamili cha uharibifu hakijajulikana bado, kwa sababu hakuna mawasiliano na sehemu zilizoathiriwa.

Mvua kubwa na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 165 kwa saa ulituwa kwenye miji hiyo. Mamata Banerjee, waziri kwenye ofisi ya rais wa India, amesema baadhi ya vijiji na miundombinu ya pwani ya Bengali magharibi viliharibiwa na kimbunga hicho cha Amphan,

Amesema wakaazi wa Culcutta wapatao milioni 15 waliamka Alkhamisi na sura nyingine ya mji wao ambao kimbunga kiliharibu paa za nyumba zao na kuwaacha wengi bila makaazi. Banerjee ameongeza kusema kuwa barabara nyingi zilifurika.

Hofu za kusambaa kwa kirusi cha Corona

Zyklon Amphan trifft Indien und Bangladesch (AFP/D. Sarkar)

Alkhamisi asubuhi kimbunga cha Amphan kiliorodheshwa katika kundi la nne kati ya tano kwenye vipimo vya Saffir-Simpson na kusababisha upepo kufikia kilomita 200 hadi 240 kwa saa. Ni kwa mara ya kwanza kimbunga cha aina hiyo kulikumba eneo la ghuba ya Bengali toka mwaka wa 1999 ambao kimbunga kingine kiliwauwa watu efu kumi kwenye jimbo la Odisha.

Zaidi ya watu milioni tatu walihamishwa na mamlaka kabla ya kufika kwa kimbunga hicho kwenye miji ya mashariki mwa India na Bangladesh, lakini hilo linaongeza mashaka kwamba makaazi ya muda yenye msongamano wa watu yanaweza kuwa kitovu cha kusambaa kwa virusi vya korona.Viongozi wamewataka raia kuheshimu kanuni za usafi na kuvaa barakoa ili kuepuka maambukizi ya kirusi cha corona.

Hii inaleta changamoto kubwa katika suala la kuwa na virusi, na pia kuhakikisha kuwa watu wako salama kutokana na dhoruba. Mashariki mwa India na Bangladesh mara nyingi hukumbwa na vimbunga  mnamo kipindi cha Aprili na Desemba na vimbunga vivyo husababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW