Uncategorized

Kimbunga Idai chazidi kuleta maafa, magari ya misaada ya kwama njiani, watu 400,000 waachwa bila ya makazi Msmubiji

Kimbunga Idai kimesababisha “janga kubwa” katika mataifa ya kusini mwa Afrika na kuathiri laki kadhaa za watu kama sio mamilioni, Umoja wa mataifa unasema.

Kwa mujibu wa shirika la habari BBC, Eneo hilo limekabiliwa na mafuriko katika sehemu nyingi na uharibifu katika nchi za Musmbiji Zimbabwe na Malawi.

Huku kukiwa na ripoti kwamba takriban angalau watu 400,000 wameachwa bila ya makaazi Msmubiji ya kati, shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linaonya kwamba huenda ikachukua siku kadhaa kabla ya athari kamili ya “janga la kibinaadamu” kujulikana dhahiri.

Maafisa kutoka kitengo cha utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya wanaonya kwamba athari ya kimbunga hicho itashuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya Afrika mashariki.

Benard Chanzu, naibu mkurugenzi katika idara ya utabiri wa hali ya hewa Kenya anasema kimbunga hicho huenda kikaathiri msimu wa mvua kwenye eneo hili.

‘Mara nyingi upepo unapovuma, kila mahali huwa unaeleka katika eneo ambapo kunashuhudiwa kimbunga kile, pahali kulipo na hewa nyepesi, upepo unapovuma unakwenda ukielekea kwenye hicho kimbunga.

‘Wakati kimbunga kimeelekea kikaja mpaka kikaktua Msumbiji, kilitunyanganya upepo wote kutoka sehemu ya Afrika mashariki, kwa hivyo inanyang’anya uwezekano wa kuwepo mvua katika sehemu hii yetu’ameeleza bwana Chanzu.

Kimbunga Idai: ‘Watu milioni 1.7 wapo katika njia kuu’ ya kimbunga Msumbiji, Zimbabwe

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ameliita “janga la kibinaadamu lenye kiwango kikubwa”.

Amesema Idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Idai nchini Msumbiji sasa huenda ikawa ya juu na kufikia watu 1000.

Kimbunga hicho kilishuka katika mji wa bandari wa Beira siku ya Alhamisi kikiwa na upepo wenye kasi ya hadi kilomita 177 kwa saa, lakini mashirika ya misaada yalifika katika eneo hilo siku ya Jumapili.

Serikali ya Msumbiji imesema watu 84 wamefariki na wengine takriban 100,000 wanahitaji kuokolewa kwa dharura karibu na mji wa Beira.

Picha ya kutoka juu ya jimbo hilo imeonyesha kiasi cha 50km ya ardhi imezikwa chini ya maji baada ya mto Buzi kuvunja kingo zake , shirika la misaada la Save The Children limesema.

Image shows a general aerial view of a damaged neighbourhood in Sofala Province, Central Mozambique
Image captionPicha ya juu ya angani ya eneo lilifonukiwa na maji baada ya mto Buzi kuvunja kingo zake

Juhudi za uokoaji zinaendeleaje?

Nchini Msumbiji, mashirika kadhaa ya misaada yanasaidia jitihada za serikali katika kuwatafuta na kuwaokoa watu na katika kutoa misaada ya chakula pia, mtandao wa ReliefWeb unaripoti.

Shirika la Telecoms Sans Frontiers limetuma maafisa mjini Beira kusaida kuidhinisha mawasiliano – ambayo yamekatizwa kutokana na mafuriko hayo – katika kusaidia kuendeleza operesheni za usaidizi.

MAP

Magari mengi ya misaada yamekwama katika barabara zilizofungika na yameshindwa kufika katika maeneo yanakoelekea. Hali hiyo imetatiza shughuli zao pia.

Taasisi ya kitaifa ya kupambana na majanga nchini Msumbiji imezipokea familia 3,800 katika jimbo la Sofala.

Shirika la msalaba mwekundu limeonya kwamba kunaweza kutokea mlipuko wa magonjwa yanayotokana na kusambaa kwa maji machafu kama vile kipindupindu kutokana na kiwango cha uchafu ulioingia kwenye vyanzo vya maji, na kutatizika kwa shughuli za kutibu maji ya matumizi.

Ndege iliyobeba misaada ilitarajiwa kuwasili Msumbiji jana Jumanne, kwa mujibu wa afisa wa shirika la save the Children aliyezungumza na BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents