Aisee DSTV!

Kimbunga Kenneth kinategemewa Tanzania na Msumbiji, TMA yatoa tahadhari wakazi wa Lindi, Mtwara na Ruvuma

Wataalamu wa hali ya hewa pamoja na Umoja wa Mataifa wameonya jana kwamba kimbunga kilicho na nguvu kinachotoka Madagascar, kinaelekea pwani ya Msumbiji na Tanzania.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Kimbunga Kenneth kitapiga usiku kucha kwa upepo mkali wenye kasi ya kilomita 80 kwa saa, hali ambayo inaweza kusababisha uharibifu mkubwa.

TMA imeongeza kuwa mikoa ya kusini mwa Tanzania ya Mtwara na Lindi iliyo karibu na mpaka wa Msumbiji ndiyo itakayoathirika zaidi na kimbunga hicho.

Mamlaka hiyo ya hali ya hewa imeonya watu wanaoishi kilomita 500 karibu na pwani wachukue tahadhari.Maafisa husika wamesema shule zote za Mtwara zimeamriwa kufungwa na watumishi wa serikali wametakiwa wabaki majumbani na kujiandaa kukabiliana na kimbunga hicho.

Malawi inategemewa kushuhudia mvua kubwa kimbunga Kenneth kitakapo piga.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW