Habari

Kimora Lee aondoka Baby Phat

Kimora Lee Simmons ameamua kuachana na Kampuni ya Baby Phat fashions miaka 14 baada ya kuianzisha akiwa na mume wake wa zamani, pamoja na mfanyabiashara mwenzake Rusell Simmons.

 

Ripoti hiyo imepatikana baada ya ‘Mogul’ huyo kuwaeleza mashabiki wake kupitia mtandao wa Twitter kwamba hataendelea kufanya kazi na Baby Phat Fashions na ingawa inasikitisha ameamua kuendelea mbele na Brand Zake nyingine zikiwemo ‘KLS’ , Kouture by Kimora na Fabulosity.

Rusell Simmons naye amempiga tafu ‘ex’ wake huyo pia kupitia mtandao wa Twitter na kuwajulisha mafans kwamba wasikate tamaa kwani yeye na Kimora wanajiandaa ku’launch’ Brands mpya na zitakuwa Kubwa kuliko.

Wengi wamekidhi kutofurahishwa na hatua aliyochukua Kimora Lee kwani Baby Phat ilikuwa kubwa na maarufu kwa sababu yake. Kuna hofu kubwa kwamba label hiyo haitaweza kuendela kufanya vizuri pasipo usimamizi wa Mwanamama huyo.

Yetu macho kwa Darubini kali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents