Burudani

Kimwana Manyele apata ulaji Twanga

Mary_Khamis

African Stars Entertainment imemchukua Mshindi wa shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis kwa ajili ya kunengua kwenye Bendi yake ya African Stars “Twanga Pepeta”. Mary Khamis amechukua nafasi ya mnenguaji Aisha Madinda aliyetimkia katika


Bendi ya Extra Bongo. Mpaka kufikia hatua ya kumchukua Mary ni baada ya kuvutiwa na kiwango chake cha uchezaji kwa kuwa alionyesha kipaji cha hali ya juu cha uchezaji katika shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 na hatimaye kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano hilo lililoisha hivi karibuni hivyo Aset ina amini hapo baadae atakuwa mmoja wa madansa hodari hapa Tanzania.

Kwa sasa Twanga Pepeta ina wanenguaji wa kike tisa na wa kiume wanne, ambao ni Abdillahi Zungu, Kassim Mohammed au Super K, Bakari Kisongo au Mandela na said Mtyanga hao ni safu ya unenguaji wa kime na kwa wanawakie ni pamoja na Fasha Sunday, Beatrice Mwangosi au Baby Tall, Asha said au Asha Sharapova, Regina Filbert, Grace Kaswaga, Vicky Pandapanda, Lillian Tungaraza au Internet, Sabrina Mathew na Maria Soloma.
ASHA BARAKA.
MKURUGENZI ASET.
picture caption.
Msindi wa shindano la Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis akionyesha funguo ya duka aliloshinda mara baada ya kuibuka mshindi. wengine Kulia ni mshindi wa pili Leila Mshana na Hawa Miraji.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents