Habari

Kinana amfagilia Rais Museveni

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema kuwa hakuna Rais aliyewahi kutembelea Tanzania mara nyingi kama Museveni(Rais wa Uganda).

Rais Magufuli amewakutanisha viongozi hao mkoani Tanga ambapo yupo na Mgeni wake Yoweri Museveni Rais wa Uganda katika uzinduzi wa Mmradi Bomba la Mafuta kutoka Hoima – Uganda hadi bandari ya Tanga.

“Hakuna Rais aliyewahi kutembelea Tanzania mara nyingi kama Museveni,alikuwa akitusihi sana kujenga reli hapa Tanga ila leo naona anafuraha kwamba reli haikuwezekana lakini bomba la mafuta limeonekana, lakini nampongeza sana Rais Magufuli kwa sera zao nzuri na vyama vyao kuwezesha bomba la mafuta,” alisema Kinana.

Hata hivyo Rais Magufuli alisema Rais Museveni anaposema ni ndugu wa Watanzania ni kweli ni ndugu kwasababu ana watoto watatu wote wamezaliwa hapa Tanzania.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents