Burudani ya Michezo Live

Kinda wa Dortmund aitamani Barcelona na Madrid kuliko kutua Man United, Guardiola yupo yupo sana Man City 

Winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, anaaminiwa kuwa anapendelea kuhamia Real Madrid au Barcelona kuliko kuhamia Manchester United au Liverpool. (Star)

Jadon Sancho, anaaminiwa kupendelea zaidi kuhamia katika timu za Real na BarcelonaJadon Sancho, anaaminiwa kupendelea zaidi kuhamia katika timu za Real na Barcelona

West Ham wanaweza kuangalia uwezekano wa kumrejesha David Moyes kama meneja wao kama watamfuta kazi Manuel Pellegrini. (London Evening Standard)

Pep Guardiola bado anapendelea kubaki Manchester City na klabu hiyo imeazimia kuendelea kuwa na utawala ”endelevu”, kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Khaldoon Al Mubarak. (Goal.com)

Wakala wa mlinzi wa Leicester Caglar Soyuncu mwenye umri wa miaka 23 amepuuzilia mbali madai kwamba ana mpango wa kuhamia Arsenal, Manchester City au Galatasaray (Leicester Mercury)

Manchester United, Liverpool, Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa timu saba zinazoongoza barani Ulaya kuwasiliana na wakala wa kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, mwenye umri wa miaka 20. (Bild, via Mail)Pep Gardiola bado ataendelea kuwa Manchester CityPep Gardiola bado ataendelea kuwa Manchester City

Mshambuliaji anayecheza katika klabu ya Rangers kwa mkopo, ambaye aliichezea England zamani katika nafasi hiyo Jermain Defoe, mwenye umri wa miaka 37, yuko tayari malipo yake yakatwe ili akamilishe mpango wake wa kuhama kutoka Bournemouth. (Football Insider)

Beki wa kati wa timu ya taifa ya Ubelgiji mwenye umri wa miaka 32, Jan Vertonghen yupo kwenye mazungumzo na klabu yake ya Tottenham kuona namna gani ataweza kuongeza mkataba wake baada ya kutua Jose Mourinho kama kocha mkuu. (Sky Sports)

Mbelgiji Jan Vertonghen anataka kujadili mkataba mpya na Tottenham

Meneja wa Tottenham Mourinho ana matumaini ya kusaini mkataba na mlizi mwingine kutoka Ubelgiji Toby Alderweireld ambaye ana umri wa miaka 30. (Football.London)

Alderweireld, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, anajihisi kuwa mwenye”bahati” kufanya kazi na Mourinho. (Talksport)Patric Vierra anapangiwa kuwa Patrick Vieira (katikati)kama kocha mkuu wa klabu ya Inter MiamiPatric Vierra anapangiwa kuwa Patrick Vieira (katikati)kama kocha mkuu wa klabu ya Inter Miami

David Beckham anatarajia kumuajiri kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Patrick Vieira kama kocha mkuu wa klabu ya Inter Miami. (Telegraph)

Kiungo wa safu ya kati anayelengwa na Manchester United na Tottenham -Bruno Fernandes, Mreno mwenye umri wa miaka 25, amesaini mkataba mpya na Sporting Lisbon ambao unajumuisha kipengele kitakachomuwezesha kuondoka kwenye klabu hiyo kwa pauni milioni 20 hadi milioni 85. (Mirror)Bruno Fernandes amesaini mkataba mpya na Sporting LisbonBruno Fernandes amesaini mkataba mpya na Sporting Lisbon

Mkurugenzi wa michezo wa Real Valladolid Miguel Angel Gomez amekiri kuwa kufanya mazungumzo na mlinzi wa Ghana Mohammed Salisu, mwenye umri wa miaka 20, ambaye anakipengele cha kumuachilia cha euromilioni 12 na amekuwa akihusishwa na Manchester United na Everton. (Sport Witness)

Celtic wako tayari kumruhusu mchezaji wa safu ya kati mwenye umri wa miaka 21, kuondoka au hata kucheza kwa mkopo mwezi Januari . (Football Insider)Muivory Coast Eboue Kouassi anaruhusiwa na Celtic kuhama timu hiyoMuivory Coast Eboue Kouassi anaruhusiwa na Celtic kuhama timu hiyo

Mlinzi wa Ufaransa ambaye Barcelona inasema haimuhitaji- Samuel Umtiti, 26, angependa kumalizia taaluma yake ya soka katika Nou Camp lakini amedokeza kwamba anataka kupata nafasi katika timu ya soka ya daraja la kwanza. (Sport)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW