Uncategorized
Kinda wa miaka 19 anayewindwa na Man United ni moto wa kuotea mbali, atupia ‘hat trick’ Europa League
Joao Felix aliweza kuitangazia dunia ubora na uwezo aliyokuwanao katika kusukuma kabumbu, ni mara baada ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’ usiku wa jana kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya Europa League na kuiwezesha timu yake ya Benfica kuibuka na ushindi wa jumla ya magoli 4 – 2 dhidi ya Frankfurt kwenye uwanja wa Estadio da Luz.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 ameripotiwa kuhitaji kwa udi na uvumba na klabu ya Manchester United.
Mshambuliaji huyo raia wa Ureno, Felix amefunga mabao yake dakika ya 21, 43 na 54 kabla ya Alves Dias kutupia la nne na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa idadi hiyo ya mabao 4 – 2.
Nyota huyo anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo katika historia ya Europa League kutupia idadi hiyo ya mabao.