Tupo Nawe

Kinda wa miaka 19 kutoka Argentina kutua Man United kwa kazi maalum, Mesut Ozil yupo sana Arsenal

Manchester United wanataka kumsaini kiungo mahiri wa Argentina Thiago Almada, 19, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal, kutoka Velez Sarsfield. (Tutto Mercato Web, via Express)

Man Utd initiate Thiago Almada transfer contact in bid to beat ...

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni kiungo mchezeshaji amefunga jumla ya mabao tisa na huku akitoa ‘assists’ nne tangu kujiunga na klabu yake mwaka 2018. Anatarajiwa kutua United kipindi cha msimu wa majira ya joto.

Kama muafaka utafikiwa baina ya pande zote mbili kati ya Red Devils na Velez, basi United italazimika kutoa kitita cha paundi milioni 22 ingawa mashetani hao wekundu wanaamini watamng’oa kwa dau la paundi milioni 16.

Mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil, 31, hataondoka klabu hiyo msimu huu na badala yake atakamilisha mwaka mmoja uliosalia katika mkataba wake na Gunners . (Fanatik, via Football London)

Arsenal wanamatumaini ya kusalia na kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos, 23, kwa mkopo hadi msimu wa sasa wa ligi ya primia utakapo kamilika, lakini wanapanga kurefusha mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania katika klabu hiyo kwa msimu mwingine. (El Confidencial, via Metro)Dani Ceballos

Arsenal wana matumaini ya kusalia na kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos

RB Leipzig wameungana na Everton katika kinyang’anyiro cha kumsaka beki wa Ufaransa wa miaka 20- Jean-Clair Todibo kutoka Barcelona. (HITC)

Manchester United bado hawajakubaliana kuhusu mkataba mpya na kiungo wa kati Angel Gomes,19, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika mwisho wa Juni. (Goal)Angel Gomes

Manchester United hawajakubaliana na kiungo wa kati Angel Gomes, kuhusu mkataba mpya

Mshambuliaji wa Benfica Carlos Vinicius analengwa na Manchester United, kiungo huyo raia wa Brazil aliye na miaka 25 anaweza kununuliwa na klabu nyingine ikiwa italipa £88m kabla ya kuanza majadiliano ya mkataba. (Sun)

Winga wa Algeria Riyad Mahrez, 29, anasema Liverpool walitaka kumsajili kabla ya ajiunge na Manchester City kutoka Leicester City lakini Reds walisitisha mpango huo walipompata Mohamed Salah kutoka Roma. (Bein Sports, via Manchester Evening News)Riyad Mahrez

Winga wa Algeria Riyad Mahrez

Chelsea wana amini watampata Charlie Webster, ambaye anaripotiwa kunyatiwa na Borussia Dortmund, katika mkataba wa wa kitaalamu atakapofikisha miaka 17 Januari ijayo. (Telegraph)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW