Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

King Kaka aeleza sababu ya kuachia Mistarillionaire

Msanii kutoka Kenya King Kaka ameeleza sababu ya kuachia ngoma yake ‘Mistarillionaire’ ambayo imetoka Disemba 31 ya mwaka jana.

Akiongea na Bongo5 bosi huyo wa lebo ya Kaka Empire amesema, wimbo huo unazungumzia maisha yake tangu alipokuwa mdogo na mageuzi yake katika mwanamuziki.

“Mistarillionaire ni mkusanyiko wa kumbukumbu na wakati ambao nimekuja kama mtu tangu huko nyuma wakati maisha yalijaribu kunihamasisha. Wakati nasema hadithi ya mageuzi ya Kaka Sungura kuwa Sungura na kwa sasa King Kaka. Pia ni hatua kwea hatua, soma kati ya mistari na uone kati ya safu,” amesema Kaka.

Wimbo huo umetayarishwa na Dan na Jack wakati video ikiongozwa na Mbayah. Tazama hapa chini wimbo huo.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW