Michezo

Kinnah Phiri: Kocha mpya Mbeya City

Kocha Mmalawi, Kinnah Phiri amesaini rasmi Mkataba wa miaka miwili kufundisha klabu ya Mbeya City ya Mbeya, ambayo imeamua kuachana na Meja Mstaafu, Abdul Mingange. Kinnah Phiri ndiye aliyefanikisha usajili wa Mrisho Ngassa klabu ya Free State ya Afrika Kusini

Kinnah-Phiri3-640x360

Hatua hii ni baada ya kuona kikosi chake kinachoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara haina mwenendo mzuri tangu kuondoka kwa Juma Mwambusi aliyekwenda kuwa Msaidizi wa Mholanzi, Hans van der Pluijm Yanga SC.

Meja Mingange aliyekuwa Msaidizi wa Mwambusi, alikua kaimu kocha Mkuu wa Mbeya City tangu Desemba, lakini sasa anaondoka moja kwa moja na Mohammed Kijuso ndiye atakuwa Kocha Msaidizi.

Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe ameiambia mtandao wa BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba wana imani ujio wa kocha huyo mwenye uzoefu utasaidia kukijenga upya kikosi chao ambacho msimu huu kimekuwa na matokeo yasiyoridhisha.
kocha huyo mpya leo jioni anatarajiwa kuanza kazi yake ya kuanza maandalizi ya kukutana na mahasimu wao Tanzania Prisons hapo Jumapili.
“Ni kweli tumepata kocha mpya, hatukuwa na amani pale timu ilipokuwa inafanya vibaya, tuliona tuna kila sababu ya kuboresha benchi la ufundi huku tukijipanga kuongeza wachezaji wengine mara baada ya msimu huu utakapomalizika,” amesema Kimbe.

Source: BIN ZUBEIRY SPORTS

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents