Habari

Kiongozi mkubwa wa upinzani aahidi kubadilisha jina la nchi, adai jina la sasa lina laana

Kama bado ulikuwa na mawazo kuwa jina la nchi haliwezi kubadilishwa kwa namna yoyote ile basi sahau hilo kwani tayari nchi kadhaa ikiwemo Swaziland na mataifa mengine duniani yamefanya hivyo na inavyoonekana kitendo hicho kimevutia baadhi ya mataifa barani Afrika.

Nelson Chamisa akiwa kwenye Kampeni

Sasa stori ni kwamba Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa ameahidi kuwa endapo atashinda nafasi ya urais atabadilisha jina la nchi hiyo na kuwa ‘Great Zimbabwe’ kwa madai kuwa jina la sasa lina laana.

Kiongozi huyo akimwaga sera kwenye kampeni za kuwania Urais nchini humo Jana Julai 16, 2018 mjini Mutare  amesema  kuwa jina la taifa hilo limelaaniwa na ndio maana taifa hilo limekuwa nyuma kwenye kila kitu.

Jina la Zimbabwe limelaaniwa hatuwezi tena kutumia jina hilo kwenye utawala wangu kama mtanipatia kura. Oneni wenyewe nchi yetu ilivyogeuzwa kuwa pagale na kila mtu duniani akiipatia picha mbaya, hatuwezi kubaki na hili jina tutakuwa tunaishi na laana iliyodumu kwa miaka mingi, mimi naiona Great Zimbabwe kwenye utawala wangu,“amesema Chamisa.

Chamisa ni kiongozi pekee wa vyama vya upinzani mwenye ushawishi zaidi kwenye uchaguzi mkuu wa urais nchini Zimbabwe unaotarajiwa kufanyika Julai 30, 2018 ambapo Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa atapambana naye kupitia tiketi ya chama tawala cha ZANU-PF.

SOMA ZAIDI – Mkinichagua kuwa Rais nitawafukuza Wachina wote-Ajinadi mrithi wa ‘Morgan Tsvangirai’

Chamisa alichukua nafasi ya kuwa kiongozi mkubwa wa chama chenye nguvu cha Upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC) baada ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Morgan Tsvangirai .

SOMA ZAIDI – Mfalme wa Swaziland, Mswati III abadilisha jina la nchi hiyo

Hata hivyo Zimbabwe kubadilisha jina lake haitakuwa stori kubwa kwani miaka ya nyuma kabla ya 1960 taifa hilo lilikuwa linaitwa Southern Rhodesia kabla ya kuitwa Zimbabwe jina linalotokana na maneno mawili “DIZIMBA” na “DZAMABWE” yenye maana ya nyumba ya mawe kwa lugha ya Shona inayozungumzwa na watu wengi nchini Zimbabwe kwa sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents