Habari

Kiongozi mkubwa wa upinzani arejea nchini Zimbabwe

Kiongozi mkubwa wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC), Morgan Tsvangirai amerejea nchini humo akitokea Afrika Kusini.

Morgan Tsvangirai

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho imesema kiongozi huyo aliwasili kimya kimya jijini Harare Jumatano ya wiki hii akitokea Afrika Kusini.

Tetesi kutoka kwenye vyombo vya Habari kutoka nchini Zimbabwe zinadai kurejea kwake kunazidisha uvumi wa kuafikiwa kwa makubaliano ya hali ya kisiasa baada ya Kuagushwa kwa Rais Robert Mugabe.

Soma na hii – Aliyekuwa Makamu wa Rais Zimbabwe arejea nchini humo

Kiongozi huyo wa upinzani amekuwa akipata matibabu ya saratani nchini Ureno na Chama chake tayari kimeeleza kuwa ndani ya masaa 24 Bw. Tsvangirai atazungumza na waandishi wa habari.

Soma zaidi – Zimbabwe hali si shwari, Jeshi lazingira kituo cha utangazaji cha taifa

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents